Ajali ya Basi yaua Huko Morogoro

Mtu mmoja aliye fahamika kwa majina ya Anthon Witike mkazi wa Dar es Salaam amefariki dunia na wengine 64 wamenusurika kifo huku 11 kati yao wakijeruhiwa vibaya kwenye ajali ya basi la abiria la Sekenke mali ya kampuni ya Kisbo iliyotokea majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Makunganya nje kidogo ya mji wa Morogoro wakati likitokea jijini Dar es Salam kuelekea jijini Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrichi Matei amemtaja dereva wa basi hilo aliyetoroka baada ya ajali na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni mwendokasi pamoaja na utelezi wa mvua ambapo amewataka madereva kuacha mbwembwe katika kipindi hiki cha mvua huku mtoto ambaye alikuwa akipelekwa kufanya kazi za ndani kuomba msaada kufuatia aliye kuwa naye kufariki katika ajali hiyo.

Wakizungumzia namna ajali hiyo ilivyotokea moja wa abiria walionusurika kifo wamesema wakati dereva akiwa mwendo kasi alijaribu kulipita lori na badaye kushindwa kulimudu hali iliyosababisha basi hilo kuacha njia na kupinduka.

Naye mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo amefika katika eneo hilo ambapo ametoa pole kwa majeruhi pamoja na ndugu wa marehemu huku akiwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ambapo kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Frances Semwene akithibitisha kuwapokea majeruhi.

Andika maoni yako hapa (MATUSI HAPANA) 
© Copyright EDDY BLOG | Edwinmoshi Official Blog | Designed By www.peruzibongo.com